Muhtasari wa IRM na mchakato wake wa kushughulikia malalamiko

Mfumo Huru wa kushughulikia Malalamiko (IRM) ni mfumo huru wa kupokea malalamiko wa Kundi la Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB au Kundi la Benki).

Ulianzishwa tangu 2006 ili kutoa msaada wa haki, huru, na wenye ufanisi (ikiwa ni pamoja na fidia) kwa watu binafsi na jamii zinazoamini kuwa zimeathiriwa vibaya au zinaweza kuathiriwa vibaya na miradi inayofadhiliwa na AfDB.

Nani anaweza kuwasilisha malalamiko?

Mtu yeyote au kikundi cha watu katika nchi moja au nchi nyingi ambako mradi unaofadhiliwa na AfDB unapatikana au una athari, ambao wanaamini kwamba wameathiriwa au wana uwezekano wa kuathiriwa vibaya na miradi inayofadhiliwa na AfDB. Kikundi kinaweza kurejelea kikundi chochote cha watu binafsi, jamii, chama au shirika. Malalamiko yanaweza pia kuwasilishwa na mwakilishi ambaye kweli ameteuliwa na watu walioathiriwa vibaya na shughuli au mradi unaofadhiliwa na Kundi la Benki.

Jinsi ya kuwasilisha malalamiko?

Hakuna umbizo maalum linalohitajika katika kuwasilisha malalamiko kwa IRM. Malalamiko yanaweza kuwasilishwa kwa:

  • Barua au barua pepe.
  • Kujaza fomu ya malalamiko mtandaoni.
  • Kutuma ujumbe wa sauti uliorekodiwa au video

Walalamikaji wanaweza kuwasilisha lalamiko lao kwa lugha yao au mojawapo ya lugha rasmi za Benki (Kiingereza, Kifaransa). Iwapo lalamiko litawasilishwa kwa lugha nyingine mbali na lugha rasmi za Benki, IRM itafanya iwezalo kutafsiri na kumfahamisha mlalamikaji kuhusu muda kadiriwa unaohitajika kwa ajili ya tafsiri. Kama lalamiko litawasilishwa kwa mdomo, IRM itawasaidia walalamikaji kuliwasilisha kwa maandishi.

Unaweza kulalamikia nini?

Lalamiko linaweza kuwasilishwa kuhusu athari yoyote halisi au inayoweza kutokea ya kijamii au kimazingira ya miradi inayofadhiliwa na AfDB.

Ni vigezo gani vinapaswa kufikiwa ili kuwasilisha lalamiko?

Wakati wa kuwasilisha lalamiko kwa IRM unapaswa kuhakikisha kwamba mradi unaolalamikiwa uko barani Afrika na unafadhiliwa kwa sehemu au wote na AfDB. (N.B. Kama huna uhakika kuhusu hili, IRM inaweza kukusaidia katika hili.) Unapaswa pia kujumuisha maelezo ya jinsi mradi unaofadhiliwa na AfDB umekuwa au una uwezekano wa kuwa na athari mbaya kwa walalamikaji au watu walioathiriwa na mradi unaowawakilisha.

Taarifa gani inapaswa kujumuishwa katika lalamiko?

Kuwasilisha lalamiko kunaweza kuwa rahisi sana. Lalamiko lazima tu lijumuishe:

  • Jina na taarifa za mawasiliano za mlalamikaji au mwakilishi (anwani, namba ya simu –simu ya mezani au ya kiganjani -; anwani ya barua pepe, n.k.).
  • Taarifa sahihi ili kusaidia kutambua utendaji kazi kama mradi unaofadhiliwa na Kundi la Benki (k.m., Jina la Mradi au Mkopaji / Mteja, eneo la Mradi na/au sekta, n.k.).
  • Maelezo ya jinsi walalamikaji wameathiriwa au wanaweza kuathiriwa vibaya na mradi; na
  • Maelezo ya juhudi zilizofanyika na walalamikaji kutaka Benki na/au Wakopaji/Wateja kushughulikia masuala yaliyo kwenye lalamiko na matokeo ya jitihada hizo, au sababu za kukwama kwa jitihada hizo.

Lalamiko linaweza pia kujumuisha taarifa muhimu zifuatazo:

Maelezo ya sera zinazotumika za Kundi la Benki ambazo zinakiukwa hasa wakati wa kuomba Mapitio ya Uzingatiaji.

  • Endapo mlalamikaji anapendelea lalamiko lake lishughulikiwe kupitia Mapitio ya Uzingatiaji au Utatuzi wa Matatizo au yote mawili.
  • Endapo usiri unaombwa na sababu za ombi kama hilo.
  • Maelezo ya matokeo tarajiwa ambayo walalamikaji wanataka kupata kupitia mchakato wa IRM.
  • Wasiwasi wowote ambao walalamikaji wanaweza kuwa nao kuhusu hatari za kulipiza kisasi.
  • Jina la mwakilishi (mtu binafsi au shirika) ambaye ameombwa kusaidia Walalamikaji na Lalamiko lao (katika hali kama hizo, Lalamiko lazima litoe ushahidi kwamba mwakilishi ameidhinishwa kutenda kwa niaba ya Walalamikaji).
  • Taarifa nyingine yoyote au nyenzo zinazohusiana na Lalamiko (nyaraka, ripoti za vyombo vya habari, ramani, picha, na nyenzo zingine za sauti na taswira) ambazo zinaweza kuwezesha IRM kushughulikia Lalamiko

Ni aina gani za malalamiko hazikubaliwi?

IRM haikubali malalamiko yaliyo nje ya mamlaka yake. Malalamiko hayo ni pamoja na madai ya udanganyifu, rushwa na/au masuala ya manunuzi. Haiwezi pia kukubali malalamiko ambayo yanawasilishwa zaidi ya miezi 24 baada ya kukamilika kwa shughuli husika, au zaidi ya miezi 24 kutoka tarehe ambayo walalamikaji walifahamu athari mbaya.

Naweza kuomba usiri / Je kuhusu masuala ya kulipiza kisasi?

Ndiyo. Unaweza kuomba usiri wakati wa kuwasilisha lalamiko kwa IRM huku ukitoa sababu za ombi hili. Iwapo kuna uwezekano wa hatari za kulipiziwa kisasi, walalamikaji wanapaswa kujadili hili na IRM ili waweze kukubaliana kuhusu njia bora ya kusonga mbele

Baada ya kuwasilisha malalamiko, ni hatua gani inafuata?

Mara IRM inapokea lalamiko, itathibitisha kupokea lalamiko hilo ndani ya siku 7 za kazi kabla ya kufanya uhakiki wa awali ili kubaini kama linaangukia chini ya mamlaka ya IRM na kukidhi vigezo vya usajili. Iwapo lalamiko hilo linastahiki, litasajiliwa na IRM itawafahamisha walalamikaji na wahusika wengine zikiwemo Bodi za Wakurugenzi wa AfDB, Rais wa Benki na Menejimenti ya Benki kuhusu hili. Kisha Menejimenti ya Benki itapewa siku 21 za kazi kujibu masuala yaliyoibuliwa kwenye lalamiko kabla ya kuwasilisha majibu yao kwa IRM ambao watawashirikisha walalamikaji majibu ya Menejimenti ya Benki na kuyachapisha kwenye Masjala ya IRM.

Baada ya lalamiko kusajiliwa na IRM kupokea majibu ya Menejimenti ya Benki, basi IRM, kwa kushauriana na mlalamikaji, itafanya uamuzi wa: 1) kutekeleza zoezi la utatuzi wa tatizo; 2) kutekeleza mapitio ya uzingatiaji / uchunguzi; 3) kutekeleza mambo yote mawili kwa wakati mmoja au mfululizo; au 4) kusitisha malalamiko kwa muda ili kumpa mlalamikaji na Menejimenti ya Benki fursa ya muda ya kushughulikia masuala yaliyoibuliwa kwenye lalamiko chini ya usimamizi wa IRM

Muda unaohitajika kushughulikia lalamiko utatofautiana kulingana na utata wa malalamiko, aina ya mbinu iliyotumika kwenye kushughulikia lalamiko, na utaratibu unaohusika katika kupata maoni ya nje kuhusu kupanga kutembelea eneo kama itabidi

Je, ninaweza kupata wapi msaada wa kuandika lalamiko langu?

Watu walioathiriwa na mradi, wafanyakazi na jumuiya zinazotafuta ushauri kuhusu jinsi ya kuandaa na kuwasilisha lalamiko wanaweza kuwasiliana na IRM wakati wowote ili kuwapa taarifa na kujadili mahitaji na Walalamikaji tarajiwa.

IRM pia imetayarisha fomu ya malalamiko kwa njia ya mtandao [katika lugha X] na barua ya mfano ya malalamiko [katika lugha X] ili kukusaidia. [WEKA VIUNGO]

Pale ambapo walalamikaji wanataka kuwasilisha malalamiko yao kwa mdomo, wanaweza kufanya hivyo kwa kuwasiliana na IRM, na tutawasaidia kwa kuweka malalamiko yao katika maandishi

Je, natuma lalamiko kwa nani?

Malalamiko yanapaswa kutumwa kwa IRM: Kwa barua Mfumo Huru wa Kushughulikia Malalamiko (IRM) - AfDB 01 BP 1387 Abidjan 01, Côte d'Ivoire Jengo la Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha Abidjan (CCIA) – Mtaa wa Jean Paul II |, Ghorofa ya 14

Kwa barua pepe: [email protected]

Kwa simu: +225 27 20 26 20 56 (Ofisi ya mbele ya IRM)

N.B .: Malalamiko yanaweza pia kutumwa kwa IRM kupitia ofisi yoyote ya AfDB nchini

N.B .: Tafadhali wasiliana na IRM kama unahitaji ushauri au maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuandaa na kuwasilisha lalamiko lako.